Wanafunzi manusura wa shule ya Lucky Vincent waamsha kilio huzuni na simanzi


Wanafunzi manusura wa ajali ya basi wa shule ya Lucky Vincent Arusha waamsha vilio , huzuni na simanzi, tukio la uwekaji wa mashaada ya maua katika mnara wa kumbukumbu wa vifo vya wanafunzi wa Lucky Vincent lililofanywa na manuaula watatu( Wilson Tarimo, Sadya Awadh na Doreen Mshana) wa ajali hiyo jana liliamsha upya vilio, uzuni, majonzi na simanzi na kusababisha baadhi ya wazazi wenye watoto waliofaliki katika ajali hiyo  kuzimia,

Jana itakumbukwa maishani mwa manusura hao kuwa ilikuwa siku ya kwanza kushuhudia mnara wa wenzao waliofaliki katika ajali hiyo uliowekwa shuleni hapo kama kumbukumbu ya wanafunzi hao, kwa kuwa wakati huo wao hawakupata nafasi ya kuaga miili au kuhudhulia mazishi yao kwasababu walikuwa wamelazwa hospitalini, juzi baada ya kutoka Marekani kwenye matibabu, Jana zoezi hilo lilifanyika shuleni hapo, hakika tuliwapenda sana ila Mungu aliwapenda zaidi wapumzike mahali pema peponi.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Saloon ya Kikie ni nini?

MAFUNZO YA USUSI WA NYWELE NA UREMBO UJUMLA (BUKOBA)

CHUO CHA UREMBO BUKOBA