Saloon ya Kikie ni nini?

SALUNI YA KIKE NI NINI?
NDUGU ZANGU LEO NAPENDA NIKUSHIRIKISHE MAANA YA SALUNI YA KIKE

Nini maana ya saluni ya kike?
       

Saloon ya kike ni nini?

             Ni sehemu safi iliyotengwa au kuandaliwa ili kutengeneza muonekano MZURI wa mwanamke au

SALOON YA KIKE ni aina ya biashara na UREMBO wa mwanamke na USUSI kwa jumla,
Biashara ya saloon ya kike ni biashara yenye changamoto kubwa sana hii ni kwasababu inahusiana na urembo,
 Ikumbukwe kuwa muonekano wa mwanamke ndio kila kitu
Kama mtu akifungua saloon ya kike hali hawezi kusuka au kutengeza nywele vizuri basi jua ya kuwa hata kama amewekeza milioni kumi saloon hiyo itakufa wakati wowote, mwanamke anapoingia saloon ya kike anakuwa anategemea apate huduma yenye kiwango kizuri na ubora atoke akiwa na muonekano mzuri zaidi yaani amependeza, kama unataka kufungua saloon ya kike usiwaze fuata hatua zifuatazo;

HATUA TATU ZA KUFUATA KABLA YA KUFUNGUA SALOON YA KIKE:

1:Jifunze kusuka na utengeneze jina :

Saloon ya kike inaanza kwa kusuka nywele mitindo tofauti tofauti kulingana na uhitaji wa mteja                                                                                                                         Mfano kusuka nywele za mikono, kushonea maweaving aina tofauti tofauti, kusokota mabutu saizi zote , kusuka yebo yebo mitindo tofauti tofauti ,
Kiujumla kusuka ndio msingi mkuu wa saloon ya kike na hili watu wakuamini na kukuachia vichwa vyao ni lazima uwe unajua KUSUKA vizuri , wanawake huenda saloon yenye msusi mzuri kwa maana hiyo kama unataka kuanzisha saloon ya kike jifunze kwanza kusuka hata kwa kuwashawishi marafiki zako ujifunzie kwao,
Pia unaweza kujifunzia kwa mtoto kwa kuharibuharibu mwanzoni ili kuongeza uzoefu au ujuzi zaidi
Ukishajua hapo ndipo unaweza kuanza kujitangaza kuwaw unasuka, kwenye kipengele hiki unaweza kujifunza mitindo ifuatayo:

Kusuka nywele za mikono
Kusokota mabutu, ya aina zote(njia mbili, njia tatu,utumbo n.k)
Kushonea weaving aina zote
Kusuka yebo aina zote
Kusuka crochet
Kusuka dread-locks aina zote(natural dread,artificial dread)
Kusuka majongoo aina tofauti tofauti
Kusuka vitunguu na zipu.

 Hatua ya pili:
2:Tafuta mtu mwenye jina akuajiri na anza kutengeneza jina kwake:

Jifunze kusuka na kisha tafuta saloon kubawa omba kazi humo na ukifika fanya kazi kama ni yako
Suka kila mtu wala usichoke ,kwa kubembelezabembeleza kupokea wateja, ongea na wateja wako vizuri , Changamka na hakikisha wateja wanakujua vizuri kuliko hata mmiliki wa saloon,anza kuchukua mawasiliano yao na tengeneza jina.
 Ukisha pata ujuzi wateja wa kutosha na mawasiliano yao basi jikusanyie mtaji:
ANZISHA SALOON ,wale  wateja watakufuata tena hata bila kelele kumbuka saloon eatu wanafuata kazi na wala sio kiyoyozi ukitengeza jina na ukawapendezesha wateja wako watakufuata popote utakapokuwa,

Hatua ya tatu:
3:Tafuta mtu mwenye jina lake muajiri,

Ili kuongeza ujuzi kwako na kuongeza wateja , kwa sababu yeye lazima atakuwa na wateja wake wengi
Fanya kazi kwa bidii na kwa ushindani hadi wateja wake wakukubali  wewe sawa  na yeye au zaidi, usikurupuke kuanzisha saloon kisha ukamuweka mtu mfano ndugu ambaye hana kazi huko kijijini au mjini na kumwajiri ili asimamie saloon, Ndugu yangu, kazi ya saloon sio kazi ambayo kila mtu anaweza kufanya bali ni kazi inayohitaji na kutegemea zaidi UJUZI.

Mfano  :  Mteja unakuta anasema , “Yule dada anaosha nywele vizuri,”. Kumbe hata kumuosha mtu nywele kunahitaji ujuzi ,wafanyakazi wengi wa saloon wanachukulia kwamba kuosha nywele ni kazi rahisi sana ikipelekea kutowaosha wateja vizuri na wakaridhika. Hivyo kama mtu hawezi kufanya kazi vizuri saloon na kwa kiwango na ubora anashauriwa kumtafuta mtu mwingine mwenye jina na wateja anayefanya kazi kwa ubora na kiwango kinachotegemewa na wateja,

Jambo la msingi hapo ukisha muajiri mtu kwako unashauriwa ukae karibu naye sana ili upate ujuzi zaidi kwake na utengeze uteja au wateja k utokana na wale aliokuja nao  na ukishafanikiwa unaweza kumwachisha kazi.
Ikiwa ulikuwa unamlipa mshahara, kwa mtu mwenye akili akishapata mtaji tu wa kuanzisha saloon yake ataondoka mapema sana hivyo unahitajika umakini wa hali ya juu sana kwa muda mfupi utakao kuwa naye. Ukishajua na kufanikisha kupata ujuzi usije ukawaza kumuachisha kazi bila maelewano au mahusiano endelevu ikiwezekana wakati anafanya kazi muandalie kiasi kidogo cha kumshukuru kwa kufanya kazi kwa uaminifu endapo itakuwa hivyo,Ili siku ukikwama ukahitaji msaada wakeiwe rahisi kukusaidia.

Mpaka hapo nilikuwa naongelea vitu viwili tu;
       @Maana ya saloon ya kike na
       @Hatua za kufuata kufungua saloon ya Kike

Endelea kufuatilia Meddy beauty Class ujifunze zaidi, tunakaribisha maswali, maoni, na ushauri, zaidi wale wanahitaji kufika Darasani kupata Practical wasiliana nasi kupitia 
0758644831 au 0629725622






Maoni

  1. Swali, ni vifaa gan muhimu vya kufungua saloon

    JibuFuta
  2. Kiukweli ukurasa wenu ni mzuri sana na mnafanya kazi kubwa awali ya yote tu niwapongezen sana sana sanaaaa

    JibuFuta
  3. Nina mwanafunzi nataka ajiunge na hapo

    JibuFuta
  4. Naomba unitext inbox au Whatsapp please nijue Nini Cha kufanya 0713354220

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MAFUNZO YA USUSI WA NYWELE NA UREMBO UJUMLA (BUKOBA)

CHUO CHA UREMBO BUKOBA